Friday 24 February 2017

MKUU WA UPELELEZI WILAYA ALIYEUAWA KIBITI ALIVYOAGWA

RPC Pwani, Bonaventura Mushongi akiaga mwili wa marehemu.
Mkuu wa Upepezi wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani, OC CID, Peter Kuponezya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana kwenye Kituo cha Ukaguzi cha Maliasili kilichopo Jaribu Mpakani, leo ameagwa na waombolezaji kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kanisani hapo.
RPC wa Ilala, Salum Hamduni akitoa heshima za mwisho.
Katika ibada hiyo walikuwepo watu mbalimbali wakiwemo ndugu jamaa na maofisa wa polisi, akiwemo Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoani Pwani, RPC Banaventura Mushongi, RPC Ilala, Salum Hamduni, Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimbo, Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Cammilius Wambura na wengineo.Afande Koba Kimanga naye akitoa heshima za mwisho.
Mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Kijiji cha Ushirombo, Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho. Marehemu ameacha mjane na watoto wawili.Ndugu wa marehem akisaidiwa wakati akimuaga mpendwa wake.Mke wa marehemu Bi. Elizabeth mwenye (kilemba) akilia kwa uchungu wakati akimuaga mumewe.Mwili wa marehemu ukitolewa kanisani baada ya ibada ya mazishi na kuagwa.
RPC Mushongi kushoto akiweka mambo sawa na makamanda wake.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.

Blog Archive