Thursday 13 April 2017

Majina ya Walimu wa Sayansi na vituo vya kazi walivyopangiwa

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017.
Share:

Rais Magufuli Akizindua Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Dar hadi Moro....Haya ni Baadhi ya Mambo Aliyoyasema

Rais Magufuli amezindua Rasmi ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Kimataifa ambayo treni ya kisasa inayotumia umeme itaweza kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

==> Haya ni baadhi ya mambo aliyoyasema
21.Unapokuwa dereva wa lori na unapopakia abiria hutakiwi kuwauliza wasimame waangalie sehemu gani, dereva mzuri anangalia kufika salama

20.Niwaombe tuangalie TZ kwanza siasa baadae, muiache Serikali ya CCM iliyoaminiwa na Watanzania itekeleze wajibu wake tutakutana 2020
 
19.Watanzania wanataka maendeleo, hakuna anayekula siasa kwa hiyo Tanzania kwanza siasa baadae

18.Tanzania tunaweza kwa hiyo tunapoyafanya haya tunafanya kwa sababu tuna wajibu wa kufanya, na haya ni malipo yangu kwenu

17.Niko kwa niaba yenu, tumeonewa sana, Tanzania ni tajiri hatutakiwi kuwa ombaomba

16.Mlinituma nifanye haya, au niwaulize ndugu zangu haya yote ninayoyafanya kweli ni mabaya?

15.Nazuia hata michanga ya madini, ninafanya kazi hii kwa niaba yenu, kwani nashindwa kusema nipelekee hiyo michanga nitaikuta Ulaya?

14.Wanasema samaki mkunje akiwa mbichi, fisadi mkunje akiwa mbichi akishakomaa mvunje, nafuu walalamike wachache, Watanzania wafurahi

13.Vita ya kupambana na ufisadi ni ngumu na hasa unapowabadilisha watu wachache waliozoea maisha fulani kwa miaka 50

12.Nataka mhandisi amalize mradi wa reli ya kisasa kabla ya miezi 30, na ikiwezekana siku ya kufungua twende bure mpaka Dodoma

11.Tunajua tunapoenda pasitokee mtu wa kubadilisha ajenda tuanze kuzungumzia ajenda ambazo hazipo kwenye ilani ya uchaguzi

10.Hivi karibuni tumepata mkopo wa kuanza kujenga barabara za mwendokasi katika awamu ya tatu na ya nne

9.Tanzania imekuwa kwa uchumi 7%, ushahidi wa kukua kwa uchumi ndio hii miundombinu tunayoijenga

8.Kazi tunazozifanya mara nyingi utakaowaona wanapiga kelele ni wale ambao walizoea kupiga dili, na mimi nataka waendelee kupiga kelele

7.Nawahakikishia Watanzania mimi ni dereva mzuri nawahakikishia lori litafika kule tunakokwenda na hili ni lori la maendeleo
 
6.Wale wataalamu wa kusoma kwenye mitandao wakaangalie ni nchi gani imejenga reli ya namna hii kwa pesa zake watakuta ni Tanzania
 
5.Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30

4.Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kutoa ajira kwa watu takribani 600,000

3.Ujenzi wa reli hii ya kisasa utasaidia kutunza barabara zetu, barabara zetu zinaharibika kwa sababu zinasafirisha mizigo mikubwa

2.Ujenzi wa reli ya kisasa utakuza sekta zingine nchini, itawezesha malighafi mbalimbali kusafirishwa kwenda kwenye maeneo ya viwanda
 
1.Ujenzi wa reli huwa ni gharama kubwa, reli hii itakuwa inabeba uzito mkubwa na spidi kubwa, watu watalala Moro na watafanya kazi DSM
Share:

Serikali yatoa ajira kwa walimu 3,081.....Yasema upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati ni 60%

Serikali imesema jumla ya walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari Omumwani Kagera, wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1.048 kati ya nafasi 4,129 za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa kibali cha ajira.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa  akizungumza na Waandishi  Habari,ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote walioajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.

Amesema walimu walioajiriwa  wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika halmashauri zote nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati.

Simbachawene amesema kati ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada  na walimu 1,544 ni wa Stashahada.

“Sehemu kubwa ya walimu wa Shahada wamepangwa  kwenye shule za kidato cha tano na sita na wachache kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’ alisema.

Simbachawene amekiri  kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na Hisabati katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

“Moja ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya sekondari ni upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati upungufu uliopo  katika shule 3,602 ni 26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248 wanaohitajika” amesema Simbachawene

Amesema walimu wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni 17,252 pekee.

Amesema kwa sasa serikali ina shule za sekondari 3,602 na kati ya hizo shule 333 ni za kidato cha tano na sita huku zingine 54 za kidato cha tano zimeanzishwa .

Aidha amesema shule hizo za sekondari kwa upande wa masomo ya Sanaa ina ziada ya walimu 7,463 ambapo waliopo ni walimu 63,240 na wanaohitajika ni walimu 55,777.

“Kutokana na ziada hiyo ya walimu wa Sanaa serikali imeanza kuchukua hatua yawahamisha walimu hao katika shule za msingi ili kuziba upungufu wa walimu katika shule hizo’’ alisema.
Share:

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.

Blog Archive