Tuesday 22 August 2017

Daktari ‘feki’ wa Muhimbili, anaswa tena Hospitali ya Amana

Mkaazi  wa  jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana.

 Juma alinaswa jana ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.

Kukamatwa kwa Juma  kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari. 

Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu  huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.
 
Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi  vya Ukimwi (WAVIU),    Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa  kwa mtuhumiwa huyo.
 
Alisema, Juma alinaswa baada ya uongozi kupata malalamiko kutoka kwa  watu waliokuwa wakihitaji huduma  katika hospitalini hiyo.

 Alisema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.

Baadhi ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na  daktari huyo feki, wamesema aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.

Nae mwananchi aliyekwenda kupata huduma hospitali ya Amana Cecilia alisema  Agosti 9 mwaka huu, kijana  huyo aliwaeleza kuwa kuna kazi  katika hospitali ya Amana na yeye kama daktari bingwa anayefanya kazi hapo anaweza kuwasaidia.
 
“Alituambia kuwa  fomu zinatolewa katika  hospitali ya muhimbili sh. 150,000 lakini kwakuwa wao ni madakatari atatufanyia kwa sh. 100,000 tu. Tulichanga fedha hiyo na ilifikia 800,000 tukampatia,”alieza Cecilia. 

Aliongeza,Juni  19 mwaka huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini hakutokea na simu akawa hapokei.

“Tuliamua kuuliza kwa madakatari kama wanamfahamu lakini hakuna aliyemfahamu ndipo tulipobaini kwamba tumetapeliwa na kuamua kufanya mtego kwa kushirikiana na uongozi uliofanikisha kumnasa  leo ,”alieleza.
Share:

Saturday 19 August 2017

MAGAZETI YA LEO TANZANIA JUMAPILI AGOSTI 20,2017


Magazetini leo Jumapili August 20,2017




MAGAZETI MENGINE TUTAKULETEA BAADAE
Share:

Thursday 17 August 2017

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.