Thursday, 2 November 2017

BOOK NOW MC ELLY NGWALA CALL +255 713 404 646 +255 767 404 647



JINA LANGU NI ELLY HEZRON MWAIFWANI NI MAARUFU KWA JINA LA MC ELLY NGWALA KAMPUNI YANGU INAJULIKANA KWA JINA LA ELLY NGWALA ENTERTAINMENT,  

NI KAMPUNI YA KIZALENDO KUTOKA NCHINI TANZANIA, INAYOJIHUSISHA NA MAMBO MBALIMBALI YANAYOHUSIANA NA BURUDANI, MITINDO, MUZIKI PAMOJA NA UANDAAJI WA MATAMASHA MBALIMBALI, KAMPUNI HII IMEANZISHWA MWAKA 2010 CHINI YA MKURUGENZI WAKE MC. ELLY NGWALA. KAMPUNI IMEKUSUDIA KUWAFIKIA WATU WENGI KATIKA KUTOA HUDUMA ZAKE ZA BURUDANI, NA KUENDELEZA UPENDO ULE ULE KAMA ILIVYO JADI YETU  WATANZANIA.


TUNAHUSIKA ZAIDI NA SHUGHULI ZOTE ZA USHEREHESHAJI (HUDUMA ZOTE ZA SHEREHE ZA KITAIFA NA KIMATAIFA ) NDANI YA ELLY NGWALA ENTERTAINMENT KUNA HUDUMA YA VIDEO PRODUCTION PAMOJA NA UPIGAJI PICHA ZA MNATO TUNAUZOEFU MKUBWA KWENYE KAZI WA ZAIDI YA MIAKA 16 .

TUMEKUSUDIA, KWAMBA IFIKAPO MWAKA 2018, TUWE TUMEKWISHA FIKA KATIKA MIKOA YA MWANZA, ARUSHA, KILIMANJARO, MBEYA, SHINYANGA NA DODOMA. NA TUTAHAKIKISHA KWAMBA HUDUMA TUNAZOZITOA ZINAISHI KATIKA MAISHA YA KILA SIKU YA MTANZANIA.
 
NINAFANYA KAZI MBALIMBALI ZIKIWEMO, MC KTK SHEREHE  MBALIMBALI, MFANO: SEND-OFF PARTY, COMMUNION, KIPAIMARA,BAG PARTY NK.
 PIA TUNATOA HUDUMA ZA VIDEO SHOOTING, STILL PICTURES, COVER DESIGN,DUBBING ZA CD,.PAMOJA NA BUSINESS PROMOTION.

MIMI NI MSHEHERESHAJI (MC) MAHIRI NA HODARI SANA KUTHIBITISHA HILI NICHAGUE NIKUENDESHEE SHUGHULI UNAYOIANDAA SASA


MC ELLY NGWALA NIKIWA KATIKA KAZI TOFAUTI AMBAZO NIMEWAHI KUONGOZA KAMA MC



FOR BOOKING PLEASE CALL
 Business No:  
+255 713 404 646
+255 784 297 582
+255 767 404 647
Email: mcellyngwala@yahoo.com

 *****Asante na Karibuni Sana*****
Share:

Monday, 9 October 2017

IGP Sirro: Sitaki Malumbano na Familia ya Tundu Lissu

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema hataki malumbano na hana majibu kuhusu shinikizo linalotolewa na Chadema na familia ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuruhusu vyombo vya nje kufanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi kwa mbunge huyo.

IGP Sirro amesema hayo jana Jumapili jijini hapa, akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alipojibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kauli yake baada ya familia ya Lissu na viongozi wa Chadema kutamka kuwa hawana imani na Jeshi la Polisi kuhusu uchunguzi huo.

Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) alijeruhiwa kwa risasi Septemba 7 mjini Dodoma na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

IGP Sirro alisema yeye na jeshi lake wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria kwa kuwatumikia Watanzania wote kuhakikisha wanakuwa salama pamoja na mali zao na si mtu mmoja.

Amewataka wanasiasa kuliacha jeshi hilo lifanye kazi yake.

"Ahsante kwa swali lakini kwa hili sina majibu kwa sababu sitaki malumbano. Sisi tupo kwa ajili ya Watanzania wote ndiyo maana nchi ipo shwari. Mimi ndiye mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na ninawajibika kuhakikisha raia na mali zao zinakuwa salama na kwa kweli ni salama. Kwa hiyo swali lako sina jibu,” alisema IGP Sirro.

Alisema ni aibu kwa mwanasiasa kutaka kumfundisha kazi askari anayetambua wajibu wake au askari kwenda kumfundisha siasa mwanasiasa, hivyo ametaka kuwe na mipaka ya utendaji kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na si vinginevyo.

Viongozi wa Chadema na familia ya Lissu imetoa msimamo ikitaka vyombo vya dola kuruhusu uchunguzi huru kwa kuhusisha vyombo kutoka nje ya nchi.

IGP Sirro yuko ziarani mkoani Mbeya  ambako amekutana na askari na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Share:

Friday, 6 October 2017

BREAKING NEWZZ:MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MANJI KESI YA DAWA ZA KULEVYA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemwachia huru mfanyabiashara, Yusuf Manji katika kesi ya dawa za kulevya iliyokuwa inamkabili.

Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema upande wa mashitaka ameshindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi yake.
Share:

Thursday, 5 October 2017

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.