Muimbaji
wa nyimbo za injili madam Flora (Zamani Flora Mbasha) amekiri kupata
mtoto nje ya ndoa yake na aliyekuwa mume wake Emmanuel Mbasha ambaye pia
ni muimbaji wa nyimbo za injili. Imefahamika.
Hilo
limefichuliwa leo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha, alipokuwa
kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook
wa EATV .
Ishu
hiyo imeibuka baada ya mmoja kati ya watu waliouliza maswali, kumtaka
Mbasha kunyoosha maelezo kuhusu mtoto wa pili wa Flora kama ni wake ama
la, na ndipo Mbasha akaweka wazi kuwa mtoto yule si wake, na Flora
mwenyewe alishakiri suala hilo.
Mbasha
amesema kuwa, Flora alikiri suala hilo hivi karibuni wakiwa katika
harakati za kuachana kwa mujibu wa sheria mahakamani, ambapo ilipofika
wakati wa kutaja idadi ya watoto aliozaa naye, Flora alimtaja mtoto
mmoja pekee ambaye ni Elizabeth (akiwa ni mtoto wao wa kwanza)
"Yule
mtoto siyo wangu, hata katika hati ya mashitaka ya kuachanishwa na
mahakama, yeye mwenyewe Flora kwa mkono wake akiwa na wanasheria wake,
aliandika kwamba kwa kipindi chote ambacho aliishi na mimi alibahatika
kupata mtoto mmoja pekee ambaye ni Eliza, kwahiyo mpaka hapo unajua
kabisa kwa hapa imeshakula kwangu, ni kitu ambacho kinauma sana, lakini
kila mtu na ujasiri wake" Alisema Mbasha.
Kuhusu
uamuzi aliouchukua baada ya kuthibitishiwa hilo, Mbasha amesema
"Nilipojua siyo wa kwangu nilikaza moyo, nikasema basi Mungu ana
makusudio yake, lakini kama ningeichukulia kibinadamu, ningeushangaza
ulimwengu na dunia"
Kuhusu
uwezekano wa kurudiana na Flora, Mbasha amesema kuwa yeye na Flora
mapenzi yao yalishakwisha kutokana na mwenza wake huyo kuamua kuanza
maisha mapya na kumuacha yeye.
Wakati
akijibu moja ya swali kutoka kwa shabiki aliyetaka kujua ni jambo gani
lililopelekea yeye kuachana na mkewe Flora Mbasha ndipo hapo Mbasha
alifunguka na kusema yeye hajamuacha mkewe, bali mkewe ndiye alimuacha
yeye kwa kumsaliti na mtu mwingine kwa sababu za kimaslahi na tamaa
kutokana na umaarufu uliowafanya waweze kuonana na watu wengi wenye
uwezo wa kila aina kifedha ikiwemo viongozi wa serikali na
wafanyabiashara.
"Mimi
siwezi kusema nilimuacha mke wangu, bali mwenzangu tayari alikuwa na
maisha mengine yaani tayari alikuwa na njia zake na alishakuwa amefanya
maamuzi na kuamua kwenda na njia ambayo yeye aliona ni sahihi na
kuendelea na maisha yake. Hivyo alinisaliti kwa sababu ya maslahi na
kwenda kwingine ambako anaona ni sehemu sahihi kwake" alisema Mbasha
Msanii
huyo anakiri kuwa kitendo hicho kilimuumiza sana na kumtesa lakini yeye
alimtumaini na kumuomba Mungu kwani hakutaka kuvuta bangi, au kunywa
pombe ili kuondokana na 'stress' bali alimuomba Mungu na Mungu
alimsaidia kupita katika kipindi hicho kigumu.
Kuhusu kuoa tena, Mbasha amesema hana mpango wa kuoa kwa kuwa hajapata mtu wa kuoa, hivyo ameamua kubaki 'single boy'
Katika
hatua nyingine amesema hawezi tena kwenda wala kuhudhuria ibada katika
Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima baada
ya kukosana na mtu mmoja ambaye hajamuweka wazi, na kwamba sasa amerudi
kwenye kanisa lake la zamani, la EAGT.
0 comments:
Post a Comment