Mbio
za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 zimezinduliwa rasmi jana katika
uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi na unatarajiwa kuzunguka
katika mikoa yote 31, ukipita kwenye halmashauri 195 kwa muda wa siku
195.
Katika
sherehe hizo za uzinduzi, kiongozi wa mbio hizo kwa mwaka huu pia
ametangazwa rasmi, ambapo atakuwa ni Amour Amad Amour kutoka mkoa wa
Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar.
Kiongozi
huyo atasaidiana na wenzake watano katika kukimbiza mwenge huo ambao ni
pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi Fatima Yunus Hassan
(Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia Mwakitalima
(Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi).
Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU'
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni makamu wa pili wa Rais wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kwa niaba ya Rais wa serikali
hiyo Dkt. Ali Mohamed Shein, ambapo katika ujumbe wake amesisitiza
umuhimu wa watanzania wote kuweka nguvu zao katika kujenga taifa la
viwanda
Alisema
hadi sasa tangu serikali yake iingie madarakani kwa muhula wa pili
tayari viwanda vitatu vya watu binafsi vimekwishajengwa visiwani
Zanzibar
Balozi
Seif alisema mbali na kaulimbiu ya mwaka huu kusisitiza umuhimu wa
viwanda, pia mbio hizo zitakuwa zikieneza ujumbe kuhusu mapambano dhidi
ya Malira, UKIMWI, Dawa za Kulevya pamoja na rushwa.
Mbio hizo zimeanzia katika wilaya ya Mpanda, na kilele chake kitakuwa ni Oktoba 14 katika mkoa wa Mjini Magharibi.
0 comments:
Post a Comment