Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli jana aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa
kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Taasisi ya
Magonjwa ya Saratani ya Ocean jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa
Watanzania kusaidia watu wenye mahitaji.
Akiwa hospitalini hapo, Mama Magufuli, alisema ameamua kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa hospitalini hapo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa yeye alizaliwa katika hospitali hiyo tarehe na mwezi kama wa huu ambapo pia alipata fursa ya kuwaombea afya njema wagonjwa wote na kuwatia moyo ndugu wanaouguza kuendelea na jukumu hilo zito.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.
Julius Mwaisalage alimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa
kujitolea kwa kusaidia wagonjwa hospitalini hapo kwa kuwa kitendo hicho
kinawatia moyo wao kama wauguzi lakini pia kinarudisha imani kwa
wagonjwa na kujiona kuwa hawapo peke yao.
Mama
Janeth Magufuli kwa kushirikiana na wanawake wa Wilaya ya Ilala na
Temeke wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema walitoa
msaada wa vitu mbalimbali kama vile mchele, maharage, sabuni za kufulia,
sabuni za kuogea, maziwa ya unga,juisi, taulo za kike, vitenge, kanga,
misuli,mafuta ya kujipaka na dawa za meno.
0 comments:
Post a Comment