Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk
Hamisi Kigwangalla amewaagiza wanaume wanaowapa mimba wanawake kutunza
mimba hizo na kulea watoto na si kukimbia na kujitokeza baada ya mtoto
kuzaliwa.
Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma alipo kuwa akijibu swali la
Mbunge wa Chakwa, Bhangwaji Meisuria (CCM) ambaye alitaka kujua baba
ataipata wapi haki ya kumwona mtoto endapo wazazi wametengana.
“Kifungu cha 26(i) kimeeleza haki za mtoto endapo wazazi watakuwa
wametengana, haki hizo ni pamoja na kuendelea kupewa matunzo pamoja na
elimu kama ilivyokuwa kabla ya wazazi kutengana, kuishi na mzazi mmoja
wapo baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa mzazi huyo anao uwezo wa kumlea
mtoto huyo,” alifafanua.
“Ninapenda kulifahamisha Bunge kuwa zipo taratibu za kufauta endapo
mzazi mmoja atakosa haki ya kumwona mtoto wake. Kwa mujibu wa taratibu
mlalamikaji anaishi na mtoto ili waweze kukutanishwa na kufanyiwa
unasihi ili hatimaye waweze kufikia makubaliano ya pamoja ya kumlea
mtoto,” alisema Kigwangalla.
Aidha Dk Kigwangalla alisema Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009
imezingatia suala zima la utoaji wa malezi, matunzo na ulinzi wa mtoto.
Na Emmy Mwaipopo
0 comments:
Post a Comment