Sunday, 1 October 2017

Nyumba ya Professor Jay yabomolewa, aeleza jinsi sheria ilivyokiukwa

Mbunge wa Mikumi Mjini, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amekumbwa na zoezi la bomoa bomoa linaloendelea maeneo ya Kimara, jijini Dar es salaam kwa kuvunjiwa nyumba yake huku akieleza kuwa uvunjaji huo haukufuata sheria.

Professor Jay akithibitisha taarifa hizo kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii amesema zoezi hilo limefanyika wakati yeye akiwa jimboni kwake na mbaya zaidi hakupewa taarifa na zoezi hilo limeendeshwa jioni ambapo sio muda wa kazi kiserikali.

“Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu. Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani.“ameandika Professor Jay huku akiwalaumu Tanroads kwa kutotoa taarifa mapema kabla ya kubomoa nyumba yake.

“Taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku Umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu. Tanesco wamenipigia simu baada ya masaa 24 au zaidi baada ya zoezi la kubomoa nyumba kufanyika kunitaarifu kuja kukata Umeme kabla ya ubomoaji huo, pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba imeshabomolewa kabisa na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu mnayoiulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu kilichokusanywa kwa pamoja na watu wa Tanroads. Tanesco walishangazwa sana kuvunjwa nyumba yangu kwa taratibu hizo.“ameandika Professor Jay.

Hata hivyo, Professor Jay amesema tukio hilo ni changamoto tu ya maisha hapa duniani na amelipokea kwa mikono yote miwili kwani kila jambo hutokea kwa sababu maalumu.

“Nimejifunza kumtegemea Na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na Naamini tutashinda“
Share:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.