Msanii mkongwe wa muziki, Mr Nice amesikitishwa na watu ambao wamemzushia kifo katika mtandao wa kijamii.
Mtandao mmoja wa kijamii uliandika taarifa za uongo kwamba muimbaji huyo amefariki akiwa nchini Tanzania.
Mr Nice ambaye yupo nchini Kenya amesema alishangaa kuona watu
wakimpigiwa simu kwa nyingi na kuulizwa kuhusu afya yake na
alivyofuatilia akagundua kuna mtandao umeandika taarifa za uongo kwamba
amefariki.
Kupitia facebook, Mr Nice aliamua kuandika taarifa hii:
East africa vibes nawashukuruni sana kwa kunizushia kifo sina la
kuwajibu ,,ila mungu awalipe kadri ya vile mnavyostaili kwa hiki
mlichonizushia leo ….mungu ni wetu sote na hasikilizi amri za binadamu
so atakaponihitaji ataniita kwa mapenzi yake but si nyie east african
vibes mnaoweza kuniua wala yeyote yule chini ya hili jua …kama nyie
hamuioni thamani yangu hilo ni juu yenu kwani huku niliko mimi ni kama
lulu na maisha yanaendelea tena kwa kiwango cha juu kabisa ..hii si mara
ya kwanza kunizushia kifo na mambo mengine ya ajabu ajabu ila all in
all mi nipo na bado mtaniona sana nikiendelea kuwepo ….im total
dissapointed kwakweli …mungu awape stahiki yenu ..THANKS SANA EATV
13/12/2016
BLOGU YA LEWIS MBONDE BLOG YASITISHA KUTOA MAUDHUI MTANDAONI
-
Kutokana na matakwa ya kisheria ya maudhiu ya kutoa huduma za kimtandao
bila kuwa na leseni iliyotolewa na mamlaka ya udhibiti wa huduma za
mawasiliano t...
6 years ago
0 comments:
Post a Comment