VIDEO Queen, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ambaye mwili wake umepungua sana kiasi cha kuwapa wasiwasi mashabiki wake, amesema licha ya kupungua huko, lakini ni mzima kwani amepima ‘ngoma’ na kujikuta yuko fi ti. Akizungumza na Risasi Jumamosi juzikati, Gigy aliifungukia afya yake na kusema baada ya kujipunguza kwa mazoezi, baadaye aliamua kutumia dawa maalum za kujipunguza kwa makusudi kwani kuna mwili aliokuwa akiutafuta na sasa umekaa mahala pake.
Gigy alisema hata hivyo, katika kuwahakikishia mashabiki kuwa kukonda kwake hakuna tatizo, ameamua kupima ngoma na majibu yamerudi yakimuonyesha yuko sawa kabisa. “Nimeamua kupima ngoma ili kuwaondoa wasiwasi mashabiki, kwani mwili huu si wa magonjwa kama watu wanavyodhani, nimejipunguza kwa kutumia dawa maalumu na nimefanikiwa nashukuru Mungu,” alisema Gigy.
Katika hali ya kushtua, Gigy pia alifungukia maisha anayotaka kwa sasa ya kutokuwa na mpenzi ‘pamanenti’ wa kupika na kupakua, badala yake anataka mwanaume atakayemuwezesha pesa tu kwa ajili ya kujikimu kisha maisha yanaendelea.
“Unajua nimegundua ukiwa na boyfriend ambaye unapika naye na kupakua, inasumbua sana na maisha yanakuwa magumu, mimi kwa sasa sitaki na wala sitarajii kuwa naye kwani hata niliyekuwa naye nimemuacha,” alisema Gigy.
0 comments:
Post a Comment