Thursday, 17 August 2017

Wanafunzi 106 watoroka usiku, wavamia sherehe na kupiga watu vibaya

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia wanafunzi 106 wa shule ya Sekondari ya Milambo kwa madai ya kufanya vurugu na kujeruhi wananchi zaidi ya sita katika eneo la jirani na shule hiyo.

Wanafunzi hao wa kidato cha sita wamefanya vurugu hizo usiku baada ya kutoroka shuleni na kuvamia kwenye sherehe ya harusi ambapo walitaka sherehe hiyo iendelee hadi muda watakao amua wao.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa wanafunzi hao 106 wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo. 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.