Hatimaye Jeshi la Polisi nchini limemwachia Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe baada ya kumshikilia
kwa saa 10.
Ofisa Habari wa chama hicho Tumaini Makene, amethibitisha kuachiwa kwa
Mwenyekiti huyo ambapo pia amesema polisi wamemtaka kuripoti katika
Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kesho Jumatano.
Mbowe aliachiwa saa saba usiku wa kuamkia leo baada ya kufanyiwa upekuzi
nyumbani kwake na kukutwa ambako polisi hawakukuta dawa za kulevya
zaidi ya nyaraka mbalimbali za chama zikiwamo Hati moja ya Chadema-Chaso
kwenda kwa Mwenyekiti ya Julai 16, mwaka 2013, picha mbalimbali nane za
matukio ya uhalifu, hati moja ya Rasimu ya Kwanza ya Chadema kuhusu
uundwaji wa Red Brigade na hati moja ya kurasa 13 inayoongelea mambo ya
Muungano.
Hata hivyo, pamoja na Mbowe kuachiwa na polisi Makene amesisitiza kwamba
kesi yake aliyomfungulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
kumtaja katika orodha ya wahusika wa dawa za kulevya iko pale pale.
0 comments:
Post a Comment