Kweli
nimeamini mapenzi hayana mwenyewe na huku waswahili husema ukistaajabu
ya Mussa…… hapo waweza malizia mwenyewe. Hii tunaiona kwa Mzee Willy
Kinyua (98) baada kufunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada ya wenza hao
kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60.
Hehehe, Wengine wetu wasipoona ndoa mapema hulalamika na kukata tamaa,
Je ungekuwa Joyce ingekuwaje baada ya kuishi na bwana huyo miaka hiyo
60, hatuwezi kusema sana ila lahasha! yawezekana mzee Willy aliupanga
huo muda ndio wakati sahihi wa kumuona Mwanamke huyo.
Wanandoa hao wamefunga ndoa katika Kanisa la Ubatizo lililopo Solai
kwenye Kaunti ya Nakuru nchini Kenya huku wakiwa na watoto 5, huku sasa
wakitembea kwa fimbo.
Aidha Kinyua alisema kuwa alikuwa miongoni mwa waliopigana vita ya
MauMau na kwamba, ingawa alikuwa porini kwa miaka tisa, Nyambura
hakumsaliti. “Nampenda Nyambura, ni mwanamke mrembo ambaye kila mara
amekuwa chanzo cha nguvu zangu na kunitia moyo. Hajawahi kunisaliti.”
Kwa upande wake Nyambura amesema, amefurahi kusheherekea ndoa yake kama
ambavyo kila mwanamke angependa iwe hivyo, huku akidai kuwa alimpenda
sana Kinyua na kwamba walikuwa wakiishi kwa imani
0 comments:
Post a Comment