RPC Pwani, Bonaventura Mushongi akiaga mwili wa marehemu.
Mkuu
wa Upepezi wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani, OC CID, Peter Kuponezya,
aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana
kwenye Kituo cha Ukaguzi cha Maliasili kilichopo Jaribu Mpakani, leo
ameagwa na waombolezaji kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili
wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kanisani hapo.
RPC wa Ilala, Salum Hamduni akitoa heshima za mwisho.
Katika
ibada hiyo walikuwepo watu mbalimbali wakiwemo ndugu jamaa na maofisa
wa polisi, akiwemo Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoani Pwani, RPC Banaventura
Mushongi, RPC Ilala, Salum Hamduni, Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi,
Advera Bulimbo, Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Cammilius Wambura na wengineo.Afande Koba Kimanga naye akitoa heshima za mwisho.
Mwili
wa marehemu umesafirishwa kuelekea Kijiji cha Ushirombo, Kahama mkoani
Shinyanga kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho. Marehemu
ameacha mjane na watoto wawili.Ndugu wa marehem akisaidiwa wakati akimuaga mpendwa wake.Mke wa marehemu Bi. Elizabeth mwenye (kilemba) akilia kwa uchungu wakati akimuaga mumewe.Mwili wa marehemu ukitolewa kanisani baada ya ibada ya mazishi na kuagwa.
RPC Mushongi kushoto akiweka mambo sawa na makamanda wake.
0 comments:
Post a Comment