Msanii
Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID, amekiri kuwa kujihusisha
kwenye utumiaji wa dawa za kulevya kumemrudisha nyuma kiuchumi.
Akiongea
kwenye kipindi cha XXL, kupitia Clouds FM Ijumaa hii, Mnyama ambaye
alikiri hadharani kuwa mmoja wa mastaa walioathirika na matumizi ya dawa
hizo, alisema hadi sasa angekuwa na utajiri wa kushangaza. Anasema dawa
hizo zina gharama kubwa.
“Nadhani
ningekuwa nimenunua kama magari mengine manane, ningekuwa nimefanya
video za muziki kadhaa zenye kiwango kikubwa. Lakini nilitumia hela
nyingi sana hasa pale ninapoenda kujirusha ningetumia hela nyingi sana,Lakini hii imefikia mwishoni,"alisema TID.
Staa huyo amedai kuwa dawa zilimfanya awe na mtazamo tofauti katika vitu vingi ambavyo alivichukulia rahisi rahisi.
“When
you are high you think you are on top, nobody can touch you sababu you
are under influence unaanza kugombana na watu, ukawajibu watu vibaya,
but when you are clean unaweza ukafanya vitu, you can save a lot of
money, you can be a better person, you can even marry a good girl, you
can fall in love,” amesema Mnyama ambaye amejitolea kuwa balozi wa vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.
“It’s over now.”
Kwenye show hiyo TID aliachia wimbo mwingine uitwao Woman ambao amedai kuwa remix yake atamshirikisha Diamond.
0 comments:
Post a Comment