Thursday 13 April 2017

Rais Magufuli Akizindua Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Dar hadi Moro....Haya ni Baadhi ya Mambo Aliyoyasema

Rais Magufuli amezindua Rasmi ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Kimataifa ambayo treni ya kisasa inayotumia umeme itaweza kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

==> Haya ni baadhi ya mambo aliyoyasema
21.Unapokuwa dereva wa lori na unapopakia abiria hutakiwi kuwauliza wasimame waangalie sehemu gani, dereva mzuri anangalia kufika salama

20.Niwaombe tuangalie TZ kwanza siasa baadae, muiache Serikali ya CCM iliyoaminiwa na Watanzania itekeleze wajibu wake tutakutana 2020
 
19.Watanzania wanataka maendeleo, hakuna anayekula siasa kwa hiyo Tanzania kwanza siasa baadae

18.Tanzania tunaweza kwa hiyo tunapoyafanya haya tunafanya kwa sababu tuna wajibu wa kufanya, na haya ni malipo yangu kwenu

17.Niko kwa niaba yenu, tumeonewa sana, Tanzania ni tajiri hatutakiwi kuwa ombaomba

16.Mlinituma nifanye haya, au niwaulize ndugu zangu haya yote ninayoyafanya kweli ni mabaya?

15.Nazuia hata michanga ya madini, ninafanya kazi hii kwa niaba yenu, kwani nashindwa kusema nipelekee hiyo michanga nitaikuta Ulaya?

14.Wanasema samaki mkunje akiwa mbichi, fisadi mkunje akiwa mbichi akishakomaa mvunje, nafuu walalamike wachache, Watanzania wafurahi

13.Vita ya kupambana na ufisadi ni ngumu na hasa unapowabadilisha watu wachache waliozoea maisha fulani kwa miaka 50

12.Nataka mhandisi amalize mradi wa reli ya kisasa kabla ya miezi 30, na ikiwezekana siku ya kufungua twende bure mpaka Dodoma

11.Tunajua tunapoenda pasitokee mtu wa kubadilisha ajenda tuanze kuzungumzia ajenda ambazo hazipo kwenye ilani ya uchaguzi

10.Hivi karibuni tumepata mkopo wa kuanza kujenga barabara za mwendokasi katika awamu ya tatu na ya nne

9.Tanzania imekuwa kwa uchumi 7%, ushahidi wa kukua kwa uchumi ndio hii miundombinu tunayoijenga

8.Kazi tunazozifanya mara nyingi utakaowaona wanapiga kelele ni wale ambao walizoea kupiga dili, na mimi nataka waendelee kupiga kelele

7.Nawahakikishia Watanzania mimi ni dereva mzuri nawahakikishia lori litafika kule tunakokwenda na hili ni lori la maendeleo
 
6.Wale wataalamu wa kusoma kwenye mitandao wakaangalie ni nchi gani imejenga reli ya namna hii kwa pesa zake watakuta ni Tanzania
 
5.Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30

4.Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kutoa ajira kwa watu takribani 600,000

3.Ujenzi wa reli hii ya kisasa utasaidia kutunza barabara zetu, barabara zetu zinaharibika kwa sababu zinasafirisha mizigo mikubwa

2.Ujenzi wa reli ya kisasa utakuza sekta zingine nchini, itawezesha malighafi mbalimbali kusafirishwa kwenda kwenye maeneo ya viwanda
 
1.Ujenzi wa reli huwa ni gharama kubwa, reli hii itakuwa inabeba uzito mkubwa na spidi kubwa, watu watalala Moro na watafanya kazi DSM
Share:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.

Blog Archive