Tuesday 21 February 2017

Mbowe Aaachiwa Huru Polisi

Image may contain: one or more people, people standing and people walking

Hatimaye Jeshi la Polisi nchini limemwachia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe baada ya kumshikilia kwa saa 10.

Ofisa Habari wa chama hicho Tumaini Makene, amethibitisha kuachiwa kwa Mwenyekiti huyo ambapo pia amesema polisi wamemtaka kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kesho Jumatano.

Mbowe aliachiwa saa saba usiku wa kuamkia leo baada ya kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake na kukutwa ambako polisi hawakukuta dawa za kulevya zaidi ya nyaraka mbalimbali za chama zikiwamo Hati moja ya Chadema-Chaso kwenda kwa Mwenyekiti ya Julai 16, mwaka 2013, picha mbalimbali nane za matukio ya uhalifu, hati moja ya Rasimu ya Kwanza ya Chadema kuhusu uundwaji wa Red Brigade na hati moja ya kurasa 13 inayoongelea mambo ya Muungano.

Hata hivyo, pamoja na Mbowe kuachiwa na polisi Makene amesisitiza kwamba kesi yake aliyomfungulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja katika orodha ya wahusika wa dawa za kulevya iko pale pale.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.

Blog Archive