Sunday 5 March 2017

Huyu Ndiye Waziri wa Mapenzi aliyeteuliwa huko Hispania kushughulikia Mapenzi




Moja ya habari iliyomake headline kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ni pamoja na hii iliyotokea Hispania ambapo Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa Waziri wa mapenzi.

Sababu zilizotajwa ni pamoja na hofu waliyonayo wanasiasa juu ya idadi ya watu inayoendelea kupungua tena kwa kasi ya kutisha.

Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa wanandoa
wanashiriki mipango ya uzazi pia hawana nafasi na wapenzi wao, hii inatajwa ndio imesababisha idadi ya watoto wanaozaliwa kupungua sana.

Aidha takwimu za hivi karibuni zimeitaja Hispania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.

Waziri wa elimu wa nchi hiyo hivi karibuni aliwasilisha ripoti yake kwa serikali kwa baraza la mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya
kwamba huenda ikaathiri Spain kiuchumi katika
miaka ijayo.

Katika kushughulikia ishu hiyo kwa haraka Waziri mkuu wa taifa hilo Mariano Rajoy amemteua Edelmira Barreira kuwa waziri anayeshughulikia mapenzi. Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na
kuuchochea umma kurudi vitandani na kusaidia
kutengeneza watoto ili kuijaza tena Hispania.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.

Blog Archive