Thursday 23 March 2017

Kauli ya Nape Nnauye Baada ya Rais Magufuli Kutengua Uteuzi Wake

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo Nape Nnauye ambaye leo ametenguliwa na Rais Magufuli amefunguka na kusema leo mchana atakutana na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.

Nape Nnauye ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mchinga amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter

"Ndugu zangu naomba tutulie! leo mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba tutulie" Nape Nnauye

Rais Magufuli leo asubuhi amefanya mabadiliko madogo ya baraza lake la Mawaziri kwa kumteua Dr. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo. ambayo ilikuwa chini ya Nape Nnauye pia amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
 
 Nape Moses Nnauye @Nnauye_Nape
Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!
Share:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.

Blog Archive