Jukwaa
la Wahariri Tanzania(TEF) leo limevitaka vyombo vya habari nchini
kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda.
TEF
wameyasema hayo leo katika taarifa yao na kulaani vikali kitendo cha
Makonda cha kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds usiku wa Machi 17
akiwa na askari wenye silaha.
“Kwa
mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul Makonda kuwa ni Adui wa Uhuru wa
Habari, na yeyote yule atakayeshirikiana naye katika kukandamiza uhuru
wa habari nchini,” ilisema taarifa hiyo ya TEF iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Theophil Makunga.
0 comments:
Post a Comment