Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo
tarehe 23 Machi, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la
Mawaziri.
Katika Mabadiliko hayo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Wateule wote wataapishwa kesho Mchana tarehe 24 Machi, 2017 Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Machi, 2017
0 comments:
Post a Comment