Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais Dkt John Pombe Magufuli juzi akiwa
yupo mkoani Dodoma, alipata nafasi ya kufanya kikao na wabunge wa chama
hicho ambapo alizungumza mambo mbalimbali ambayo hafurahishwi nayo kama
kiongozi mkuu wa chama.
Rais
Magufuli alikutana na wabunge hao katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani
Dodoma ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumza nao ni pamoja na
kuwaambia kuwa anafahamu baadhi ya wabunge wanampinga Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa.
"Nafahamu
baadhi yenu mnampinga Waziri Mkuu na mnataka aondolewa kwa kura ya
kutokuwa na imani naye, naomba niwaambie kuwa hamtafanikiwa. Mimi
namuunga mkono msaidizi wangu huyuo kwa asilimia 100 kwa nimejionea
mwenye namna anavyoweza kufanya kazi, "alisema Rais Dkt Magufuli na
kuongeza.
"Hata
mkimuondoa, nikija kuteua mwingine nitamleta huyu huyu na endapo
mtamkataa basi nitavunja bunge wote mrudi kwenye uchaguzi."
Mbali
na hilo kiongozi huyo alitoa onyo kwa wabunge wa CCM ambao wanagawa
muda wao wa kuzungumza na kuwapa wabunge wa upinzani pindi wanapokuwa
kwenye vikao vya bunge.
Kauli
hii imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Boniface Getere
kumpa dakika tano mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba kutoka
kwenye muda wake wa kuchangia ambao ni dakika 10.
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti Dkt Magufuli amewaambia kuwa anakerwa na
baadhi ya wabunge kufifisha jitihada za serikali katika kupambana na
dawa za kulevya huku akimtuhumu mbunge mmoja kutoa siri na kuzipeleka
upinzani.
Kuhusu
matangazo ya bunge kutokurushwa mubashara, Mwenyekiti wa CCM aliwaambia
wabunge hao kuwa yeye ndio aliamua iwe hivyo kutokana na wabunge wengi
kuwa wapiga porojo tu.
Credit: Mwananchi
Credit: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment