Mwanamuziki
Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego amekamatwa na Polisi leo
asubuhi mkoani Morogoro na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero
mkoani humo.
Nay
wa Mitego amekamatwa akiwa hotelini Morogoro baada ya kuamaliza
shughuli zake zilizompeleka ambapo alitakiwa kuongozana na polisi hao
hadi kituo cha polisi.
“Nimekamatwa
kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu
iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police. Nawapenda Watanzania wote.
✊🏿✊🏿 #Truth #Wapo.” Ameandika Nay wa Mitego kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Licha
ya kuwa mwanamuziki huyo hajaeleza sababu ya kukamatwa kwake, au Jeshi
la Polisi kutoa taarifa, lakini inaaminika kuwa sababu kubwa ni wimbo
wake alioutoa siku za hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Wapo.
Wimbo
huo umezungumzia mambo mengi hasa ya kisiasa yanayoendelea nchini kwa
sasa ikiwa ni pamoja na tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda, uhuru wa vyombo vya habari na masuala ya sanaa.
0 comments:
Post a Comment