Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe,
ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego aliyekuwa
akishikiliwa na Jeshi hilo.
Mwakyembe
amesema Rais John Magufuli ameruhusu wimbo wa Ney wa Mitego"WAPO"
upigwe vyombo vyote na pia uongezewe vionjo ikiwemo rushwa na mengine.
Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo
huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Akiongea
na Wandishi wa Habari muda huu mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata
Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii
huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa
Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na
maadili mema katika jamii.
0 comments:
Post a Comment