Waziri Nape: Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda
Waziri Nape: Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itasomwa wazi
Waziri Nape: Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru. Mamlaka zitajua cha kufanya
Kusaga: Kama RC Makonda ataomba radhi hatuna shida naye, ataendelea kuwa rafiki!
Reginald Mengi: Tuna Rais anayependa Vyombo vya Habari, lakini mapenzi haya ayaonyeshe kwa Vitendo!
Nape Nnauye(Waziri wa Habari): Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi
Nape: Natoa pole kwa Clouds Media na kwakuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia
Nape Nnauye: Ripoti itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24
====
Habari zaidi....
Waziri Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye
amesema kuwa Tukio la Uvamizi wa Kituo cha Habari cha Clouds unaodaiwa
kufanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul makonda akiwa na
askari kadhaa ni tukio la kupingwa huku akidai kuwa matukio kama hayo
hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa lakini kama Rais yupo, nchi
haijapinduliwa.
Aidha amesema kuwa Vitendo hivyo ni kunajisi uhuru wa habari na kama
akishindwa kusimamia hilo na yeye hafai kuwa katika nafasi aliyopo.
Chanzo : Mwananchi
BLOGU YA LEWIS MBONDE BLOG YASITISHA KUTOA MAUDHUI MTANDAONI
-
Kutokana na matakwa ya kisheria ya maudhiu ya kutoa huduma za kimtandao
bila kuwa na leseni iliyotolewa na mamlaka ya udhibiti wa huduma za
mawasiliano t...
6 years ago
0 comments:
Post a Comment