Walimu wakuu wa shule za msingi Magunga na Lubanta, Wilaya ya
Mvomero zilizofanya vibaya kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka jana,
wamekabidhiwa kinyago.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly alikabidhi kinyago hicho
katika tukio lililoshuhudiwa na walimu wakuu wa shule za msingi na
waratibu elimu kata wa wilaya hiyo, shule hizo zitakaa na kinyago hicho
kwa kupokezana ndani ya miezi sita kila shule.
Shule zilizofanya vizuri zimepatiwa vyeti maalumu vilivyosainiwa na
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ili
ziongeza bidii.
Ofisa Elimu ya Msingi wilayani Mvomero, Michael Ligola alisema
kutokana na wilaya hiyo kufanya vibaya kitaaluma katika matokeo ya mwaka
jana, walifanya utafiti mdogo wa kuzunguka kwa baadhi ya kata kuona
kilichosababisha hali hiyo.
Ligola alisema asilimia 80 ya matatizo waliyoyabaini katika maeneo
mengi uwezo wake upo ndani ya maeneo husika, ikiwamo kuwahusisha wakuu
wa shule na waratibu.
Source: Mwananchi
Source: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment