Thursday, 23 March 2017

Viongozi, mastaa watoa maoni yao kufuatia Nape kupokonywa uwaziri, wengi wamuita ‘shujaa

Mshtuko huo umetokana na taarifa ya mheshimiwa Nape Nnauye kupokonywa nafasi ya uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hii imekuwa habari yenye mpasuko mkubwa hasa katika kipindi hiki ambacho Nape ameonekana kuwa mtetezi muhimu wa vyombo vya habari kufuatia kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha nzito.
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kupokea ripoti toka kwenye kamati aliyokuwa ameiteua kufanya uchunguzi wa tukio hilo, Nape ameondolewa na kuacha sintofahamu kubwa kwenye mkasa huo.
Mastaa, viongozi na wananchi wametoa maoni yao ambao mengi yanafanana – hawajependezwa na kilichotokea huku wengi wakimwelezea Nape kama shujaaa.
Haya ni baadhi yao:
Zitto Kabwe
Nimezungumza na mbunge wa Mchinga @Nnauye_Nape na kuthibitisha kuwa Ni Kweli ameondolewa kwenye Uwaziri. Nape ni Shujaa wa kizazi chetu
Irene Kiwia
The key resource of ordinary citizens is numbers. And justice will reign on earth and truly will the voice of the people be the voice of God. When there is true awakening of the people, in numbers, it forms the real and conscious public opinion.
B12
Nitakua naota eti……. Ngoja nilale tena then niamke! Maana hii si mara ya kwanza kukutana na ndoto mbaya ya kutisha!!
Nchakalih
Kaka @Nnauye_Nape nakushukuru kwa kunipa mfano wa kutumia kumfundishia mwanangu zion somo la uzalendo! HISTORY will JUDGE you RIGHT!!
Halima Mdee
Naamini ni UZUSHI!!
Edo Kumwembe
Sidhani kama Nape anajali…alilitafuta hili kwa nguvu zote…sidhani kama anajali

Bonge la Nyau
Huyu ni shujaa wangu……
Wema Sepetu
We will Surely Miss U as Our Minister… Tulishakuzoea. Such a way to start Your Morning.. Lets wait for what’s NEXT…. This Is Tooo Much Jamani. This Country Be Full of Surprises Nowadays…. Smh.. Never Knew Nchi ina MaRais wawili… Now I know…. Smh…
Idris Sultan
Raisi akashika Jiwe na Almasi akavipimaaaaaaaa aksema embu katupeni almasi ina’ngaa kijinga jinga tu nimeiambia ing’ae kwani.
Madee‏
Sad newz
Masoud Kipanya
Haya ni mawazo yangu… Ningekuwa @Nnauye_Nape ningekaa KIMYA kabisa
Diva
Nimepata mshtuko wa mwaka . Kama Kijana Mpenda Haki na Mpenda Maendeleo na Ninaejitegemea Nimepata Mshtuko wa Mwaka , Nimejiuliza maswal Kwa uchungu Chozi limetoka
Peter Msigwa
Kwa Magufuli bashite ni mhimu na ni bora kuliko Nape ndani ya chama na serikali! Hongera JPM!
Mwana FA
(Alitweet muda mfupi kabla ya habari za kuondolewa uwaziri (Toka mwanzo kabisa wa haya maswahibu,kaka yangu @Nnauye_Nape anaonesha ukomavu wa hali ya juu kabisa..kisiasa na kibinadamu. Anajua umuhimu wa kufanya ‘vita’ dhidi ya mambo yasiyo sahihi kwa jamii bila dhulma na ukiukwaji wa sheria,na hayumbi kwy kusimamia ukweli.
NA HARINGI ..SALUTE kaka @Nnauye_Nape …najivunia kusema nakujua,ubarikiwe ndugu yangu)
Baada ya habari hiyo kufahamika alitweet: Aisee..
Aika
Its not dictactorship its being a coward #JustSaying running frm people challenging u

Quick Rocka
I don’t feel proud kuwa mtanzania anymore….Tunatangazaje na kusifia nchi ambayo viongozi wanaosimamia ukweli na sheria wanaondolewa…Huku wanaozingua wanaendelea kupeta…Nape alikuwa waziri sahihi kabisa kwetu wasanii,wanamichezo na wanahabari.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

MC ELLY NGWALA

FOR BOOKING PLEASE CALL Business No: +255 713 404 646 +255 784 297 582 +255 767 404 647 Email: mcellyngwala@yahoo.com

MC ELLY NGWALA KTK POZI

My Blog List

Powered by Blogger.

Blog Archive