Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kwa sasa amepumzika na anafurahia maisha ya kustaafu kwake.
Alizungumza hayo mjini Dodoma katika mkutano maalum wa CCM, alipopewa
nafasi ya kuzungumza, pamoja na kufurahia ustaafu wake pia alifurahia
ukumbi kupewa jina lake.
Alisema huku akishangiliwa “Nimepumzika na-enjoy (nafurahia) maisha ya kustaafu.”
Sambamba na kufurahia kustaafu huko alizungumzia mabadiliko
yaliyofanyika ndani ya chama hicho alisema yataongeza ufanisi katika
chama hicho na kuwataka wanachama kutokuwa na hofu.
Alisema mabadiliko hayo yatasaidia chama hicho kuweza kujiendesha
ikizingatiwa changamoto mojawapo ya chama hicho ni gharama kubwa za
uendeshaji huku vyanzo vyake vya mapato vikiwa ni ada za uanachama na
kuuza mali za chama.
“Tuna wanachama milioni nane, kama wote wangekuwa wanalipa ada
tungekuwa na uhakika wa Shilingi bilioni 12 na kungekuwa hakuna cha
kutuhangaisha tukiongeza na ruzuku zetu.”
“Lakini kwenye ada unakuta tunapata Shilingi milioni 500 tu, gharama
za mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ni Shilingi milioni 600, hivyo
lazima rais ahangaike kusaidia,” alisema Kikwete.
By: Emmy Mwaipopo
0 comments:
Post a Comment