STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameibuka na
kusema kuwa endapo itatokea muziki ukambumia atageukia kazi ya mama
ntilie ‘mama lishe’ kwa sababu anaipenda na iko kwenye damu.
Akibonga na Risasi Jumamosi, Shilole alisema tangu akiwa mdogo
anapenda sana kupika hivyo hata sasa pamoja na kufanya muziki amekuwa
akipika mwenyewe kwenye mgahawa wake aliofungua hivyo ikitokea kazi ya
muziki imekataa atageukia kabisa kwenye kazi ya mama lishe kwani
anaiweza na inalipa kuliko kawaida.
“Sioni aibu kuwa mama lishe maana ni kazi ninayoipenda
na nikiacha muziki ndiyo itakuwa kazi yangu maalum sitahangaika na vitu
vingine, sioni aibu kufanya kazi hiyo maana sina tabia za kuigiza maisha
kama mastaa wengine, hapa penyewe huwa napika mwenyewe
ili kuwafurahisha wateja wangu, namshukuru Mungu kazi hii inalipa kwani
fedha ninazopata kwenye muziki huwa naziwekeza kwenye mtaji huu wa
mama lishe,” alisema Shilole.
Chanzo:GPL
0 comments:
Post a Comment