Aliyekuwa
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ameibuka na kuongea mambo
matano kuhusiana na sakata la vyeti feki linalomuandamana Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kafulila amesema yafuatayo;
"Kwanza
ni ushauri wangu kwamba Makonda amsaidie Rais ama kwa kuonesha vyeti
vyake vyote kuondoa utata au ajizulu ili serikali iendelee na mambo
mengine.
"Obama alipotuhumiwa kuhusu uraia wake USA alifanya kazi ndogo tu ya kuweka vyeti vyake vyote hadharani na akawa amefunga utata wa uraia wake. hivyo ni vema Makonda afanye hivyo kama anavyo au akae pembeni kwani nchi ni muhimu kuliko mahusiano yake na Rais.
"Obama alipotuhumiwa kuhusu uraia wake USA alifanya kazi ndogo tu ya kuweka vyeti vyake vyote hadharani na akawa amefunga utata wa uraia wake. hivyo ni vema Makonda afanye hivyo kama anavyo au akae pembeni kwani nchi ni muhimu kuliko mahusiano yake na Rais.
"Rais
anapaswa kujua kuwa hoja ya jinai ya kughushi vyeti inayopigiwa kelele
inahusu pia umakini wa mamlaka yake kama mteuzi wa Makonda kwamba kuna
shida ya vetting. hivyo kuondoa hilo ni kuchukua hatua stahiki. hakuna
namna Rais atamlinda Makonda na akabaki na sifa ya kuwa Rais anaesimamia
haki na Usawa. Itafanya aonekane kama waliomizwa na ukali wake katika
kusimamia sheria ni kwasababu hawakuwa na ukaribu nae na zaidi itafanya
aonekane Rais wa kawaida sana kwa kulinda uovu kwa sababu za
binafsi.Hivyo ukimya wa Rais unafanya dhamira yake ya uzalendo ihojike
kwani sio kawaida yake.
"Mamlaka
kama Sekretariet ya Maadili ya Uongozi ilipaswa kuwa imeshachukua hatua
kuondoa wingu hili kwani kinachojadiliwa hapa mbali zaidi ya jinai pia
kinahusu uadilifu wa Kiongozi(intergrity). ukimya wa taasisi hii ni
mfano mbaya wa namna taasisi zinavopigwa ganzi pindi haki inapotakiwa
kutendeka lakini inagusa maslahi ya Rais. huu ni uzoefu niliopata kuona
hata kwenye sakata la Escrow.likitokea jambo ambalo Rais ana maslahi
taasisi zetu zimekuwa nzito na kigugumizi kuchukua hatua ipasavyo.
"Chuo
cha Uvuvi walichomsajili kwa cheti cha form4 ambacho anatuhumiwa kuwa
sio chake pamoja na Chuo Kikuu ni taasisi ambazo mjadala huu unahusu
heshima ya taasisi hizo. hivyo ilipaswa zijitokeze kuthibitisha au
kukanusha. ukimya wao unaashiria hofu yao kwasababu kaguswa mtoto wa
mfalme! Huu ni mfano mbaya kabisa kwa taasisi za taaluma kwamba zinaweza
kuwa za hovyo kiasi hiki.
"Kibaya
zaidi ni ukimya wa NECTA ambao ni mamlaka ya kutoa vyeti. sasa cheti
kinachosumbua hapa ni cha form4 ambacho ni mali yao. lakn kwa woga
wamekaa kimya kuficha ukweli na kuacha mjadala wa cheti uwe kati ya
Askofu na RC na watanzania wakati wao ambao ni mamlaka sahihi kuondoa
utata wamekaa kimya kwa hofu ya kugusa mtoto wa mfalme.. Hili ni
fundisho la kwani nchi hii haiendelei kwasababu taasisi hizi haziko
imara kutimiza majukumu yake kisheria bali zinafanya majukumu yake kwa
kadiri ya mapenzi ya mteule wao."
0 comments:
Post a Comment