Aliyekuwa
Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo Nape Nnauye ambaye leo
ametenguliwa na Rais Magufuli amefunguka na kusema leo mchana atakutana
na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
Nape Nnauye ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mchinga amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter
"Ndugu
zangu naomba tutulie! leo mchana nitakutana na Wanahabari na
tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba tutulie" Nape Nnauye
Rais
Magufuli leo asubuhi amefanya mabadiliko madogo ya baraza lake la
Mawaziri kwa kumteua Dr. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Sanaa
utamaduni na michezo. ambayo ilikuwa chini ya Nape Nnauye pia amemteua
Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na
Sheria.
Nape Moses Nnauye
✔
@Nnauye_Nape
Ndugu zangu
naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza
hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!
0 comments:
Post a Comment