Baada
ya Yanga kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 na Zanaco FC ya Zambia
kwenye mchezo wa klabu bingwa Afrika uliochezwa uwanja wa taifa
Jumamosi March 11, 2017, watu wameongea mambo mengi sana, miongoni mwao
ni afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara.
Manara
ame-post ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwaita Yanga
wasindikizaji huku akisema watu wasubiri kupata burudani mwaka ujao
kutoka kwa Simba.
“Wasindikizaji
safari yao imeshaiva, ni kujipanga tu na TAZARA kwenda kukamilisha
ratiba. Tungoje mwakani mnyama atatupa raha wabongo,” maneno
yanayosomeka kwenye account ya Instagram ya Manara.
Simba
inaweza kufuzu kucheza michuano ya kimataifa (Caf Champions League au
Confederation Cup) ikiwa watashinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara au
ubingwa wa Azam Sports Federation Cup.
Hadi
sasa Simba bado ipo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa mataji hayo
yanayosimamiwa na TFF. Inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi mbili huku
zikiwa zimesalia mechi mechi sita huku ikiwa imefuzu kucheza robo
fainali ya ASFC.
0 comments:
Post a Comment