Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Jumanne hii ameanza
kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu
tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge.
Kwa mujibu wa maelezo kwenye akaunti maalum ya Facebook ya bunge
hilo, wito wa kufika mbele ya kamati hiyo umefikiwa kufuatia azimio la
Bunge kumuomba Mhe Spika kuwaita mbele ya kamati wakuu wa wilaya na
mikoa waliotoa matamshi ya kudharau mamlaka ya Bunge.
0 comments:
Post a Comment