Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego amefunguka mengi mbele ya
waandishi wa habari muda mchache baada ya kuachiwa na jeshi la polisi.
Rapa huyo alishikiliwa na jeshi hilo kwa siku mbili baada ya wimbo wake mpya ‘Wapo’ kuonekana hauna maadili.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kutoka kituo cha polisi
alipokuwa akishiliwa, Nay ameishukuru serikali pamoja na wadau
mbalimbali ambao walikuwa wanampambania.
“Nawashukuru sana watu wa media, wanasheria wangu ndugu jamaa na
marafiki kwa upendo waliouonyesha kwangu. Pia naishukuru serikali kwa
hichi walichokifanya, sasa hivi sina kubwa la kuongea wimbo umeruhusiwa
nashukuru na nimefurahi kusikia hivyo,” alisema Nay wa Mitego.
Rapa huyo amesema kwa sasa anajipanga kufanya maandalizi ya kuandaa video kwajili ya wimbo huo.
Katika taarifa iliyotolewa mapema leo na Rais Magufuli alisema wimbo
huo ni mzuri lakini aongezee changamoto nyingine zilizopo kwenye jamii.
0 comments:
Post a Comment