MWENYEKITI wa CCM, Rais John Pombe
Magufuli, (pichani wapili kushoto), akiongoza kikao cha Kamati Kuu (CC),
ya chama hicho kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
almaarufu kama White House, leo Machi 11, 2017. Katika kikao hicho,
viongozi wengine wa juu wa CCM waliohudhuria ni pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa CCM, (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein,
Makamu Mwenyekiti wa CCM, (Bara), Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, Makamu wa Rais, Samia Sukluhu Hassan, Makamu wa pili
wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Seif Iddi, Spika wa Bunge, Job Ndugai,
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zuberi Ali Maulid. Kikao hicho
kitafuatiwa na kile cha Halmashauri Kuu, (NEC), kabla ya Mkutano Mkuu
Maalum utakaoanza kesho Jumapili Machi 12, 2017, ambao jukumu lake kubwa
ni kupitisha mabadiliko ya katiba ya chama hicho ya mwaka 1977 pamoja
na kanuni zake.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kumpa nafasi
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk JohnMagufulikufungua na kuongoza kikaocha
Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. Kushoto ni Dk. Shein na Kulia ni
Mangula.
Wajumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo na Shamsi Vuai Nahodha
wakibadilishana mawazo kabla ya kikao hicho kuanza leo mjini Dodoma.
Wajumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo na Shamsi Vuai Nahodha
wakibadilishana mawazo kabla ya kikao hicho kuanza leo mjini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akisalimiana na Spika wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulidikabla ya kuanza kikao
hicho. Katikati ni Spika wa Bunge Job Ndugai
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kikao hicho. Kushoto ni Katibu
wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Seif Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Vuai Ali Vuai
Mwenyekiti wa CCM, Rais John Pombe
Magufuli, akipokewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana,
(kushoto), wakati akiwasili makao makuu ya chama hicho kuongoza kikao
cha Kamati Kuu na kile cha Halmashauri Kuu mjini Dodoma Machi 11, 2017.
(PICHA NA BASHIR NKOROMO)
0 comments:
Post a Comment